Leo tarehe 11 January 2014, kulikuwa na kikao
kilichowahusisha wawakilishi wa masomo chuo kikuu cha elimu mkwawa
kilichoitishwa na kamati ya Elimu na Taaluma ya Bunge la DARUSO MUCE. Kikao kilichoanza
mnamo saa 11:00 Asubuhi. Kikao kilianza kwa mwenyekiti wa kamati Mh. Frank
kukaribisha maoni ya wabunge na baadae kumkaribisha waziri wa elimu Mh Ephraim Jonas kutoa
ufafanuzi juu ya msuala mbalimbali. Masuala yaliyozungumzwa na kutolewa ufafanuzi ni kama ifuatavyo:-
1. suala la uhaba wa viti. wabunge walihoji uhaba wa viti hasa katika kumbi za mihadhara ya AH, CF na RL 7. Waziri wa elimu alijibu hoja hiyo kwa kusema "Suala hilo linashughulikiwa na utawala na tayari wameagiza meza 500 na viti
2. Suala la vyumba vya kusomea kuwa vichache, pia waziri alisema "kuna lecture theaters zitafunguliwa kuanzia semester ijayo, na moja ya ukumbi mkubwa kabisa utakaochukua watu 800 kwa pamoja utaanza kutumika kuanzia semester ijayo katika eneo la majengo mapya karibvu na office za finance".
3. Suala la Prospectus kwa mwaka wa pili, pia lilizungumzwa na wabunge hao ambao walitaka wapewe prospectus ikiwa ni haki yao na ni njia rahisi ya wao kujifunza na kupunguza maswali juu ya masuala mengi ya kitaaluma. pia prospectus ni moja ya kumbukumbu katika maisha kuwa aliwahi kupata elimu katika chuo hiki na walifundisha na walimu wapi. waziri aliahidi kuendeleza ushawishi ili mwaka wa pili wapate prospectus. pia alisisitiza kutopatatikana ni sababu ya kubadilishwa kwa utaratibu wa ku major na ku minnor ulioanza mwaka 2012
4.Suala la computer. Wabunge walihoji juu ya baadhi ya komputa
kutotumika kama vile zile za maktaba, na chumba cha komputa waziri alidai kuwa
komputa za maktaba bado mkandalasi hajamalizia kufunga vifaa kwa ajili ya
kuanza kutumika, na hivyo suala lipo kwenye utekelezaji muda si mrefu, pia
suala la chumba cha komputa mchakato wa ununuzi wa vifaa umeshafanyika hivyo
zitatengenezwa muda si mrefu.
5.Suala la wireless internet na internet cable. Wabunge waliomba
kuanza kutumika kwa wireless internet katika maeneo ya chuo, na walisisitiza
juu ya kutumika suala la internet cable kwa ajili ya komputa mpakato. Waziri alijibu
kuwa ataendelea kufuatilia ili masuala hayo yafanyiwe kazi na utawala.
6. Suala la kelele. Kwa pamoja wabunge waliazimia kuwataka
wanachuo hasa wale wanaopokea simu kwenye Seminar rooms na lecture rooms kuacha
tabia hiyo ambayo ni kero kwa wanachuo wanajisomea maeneo hayo, pia suala la
kufanya mijadala walikumbushia kuwa mijadala yote lazima ifanyike AH, CF na LR
7 na maeneo ya vimbweta tu na si SR wala LR.
Hayo ndiyo masuala yaliyochukua uzito mkubwa, pia masuala
mengine yalikuwa ni Chuo kiongeze rasimali watu kwenye sehemu mbalimbali ili
kuongeza ufanisi wa masuala mbalimbali kama vile usajili, na ufundishaji wa
vipindi kwa kupunguza walimu wa muda (part-timers). Mbao zifutwe mara kwa mara.
Pia waliomba kupata nafasi ya kukutana na wawakilishi wa utawala ili
kuzungumzia masuala mbalimbali yanayowakumba wanachuo kwa ujumla.Hayo tu ni baadhi ya masuala mengi yaliyo zungumziwa
Hizi ni baadi ya picha za wajumbe wa kikao hicho katika
tukio hilo
Imetolewa na waziri
wa habari
DARUSO MUCE 2013/2014
AGUSTINO ALPHA
nyie mnanenepa 2 hamna lolete ukicheki waziri mkuu kawa tukunyema raisi ndo usiseme
ReplyDeleteutekelezaji muhimu!
ReplyDeleteTHANKS MUCH DARUSO-MUCE!
ReplyDeleteI SEE NOW THE WIRELESS INTERNET IS AVAILABLE FULLEST.
_______
By,
Sylvester, Raymund
+255 684 750 153 or rstweve@gmail.com