Sunday, December 08, 2013

KWA WANACHUO WANAOISHI NJE YA CHUO



Wabunge wa jimbo la Mkwawa-Makanygio na Ilala. Wanapenda kuwataarifu wanachuo wote wanaoishi nje ya chuo kuwa,
Kumekuwa na taarifa za wizi uliokithiri kwa wanachuo waishio nje ya chuo, hasa katika msimu huu wa sherehe za mwisho wa mwaka.
Baada ya kupokea taarifa na kwakushirikiana na Wizara husika ya nje wameomba ridhaa kwa Dean of students ya kufanya kikao na Afisa mtendaji kata ya Mkwawa na Wenyeviti wote  wa  Serikali za Mitaa. Baada ya Dean kuona uzito wa suala lenyewe ameruhusu kufanya kikao, na sasa inasubiriwa ofisi ya Dean kufanya mawasiliano ya Kikao hicho cha viongozi na ofisi ya Afisa Mtendaji kata.
Baada ya kufanyika kikao hicho cha viongozi na ofisi ya Afisa Mtendaji, Viongozi watatoa taarifa ya kikao cha mrejesho kwa wanachuo wote wanaoishi nje ya chuo.
Kwa kipindi hiki wakati taratibu zinaendelea kufanyika ni vema kila Mtu awe makini yeye pamoja na mali zake.
Wenu wawakilishi; 
  08/12/2013
      CHIPETA,  Alfonce (Mb)- Mkwawa Makanyagio. 0754 393 752.
       IKENDA,  Ambele (Mb)- Ilala. 0769 851 449
      

No comments:

Post a Comment