DR. SIMON LYUBA, MGANGA MKUU WA KITUO CHA AFYA CHUO KIKUU
CHA MKWAWA ANAPENDA KUWATANGAZIA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI. TAREHE
1.12.2013
Tarehe 1.mwezi wa desemba ni siku ya UKIMWI duniani na
maadhimisho ya siku hiyo kwa manispaa ya iringa yatafanyika kwenye viwanja vya
mpira chuo kikuu cha mkwawa
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “TANZANIA BILA MAAMBUKIZI MAPYA,
UNYANYAPAA UBAGUZI NA VIFO VITOKANAVYO NA UKIMWI INAWEZEKANA”
Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa
Wanajumuiya wote wa chuo kikuu cha mkwawa mnakaribishwa sana
(wanafunzi na wafanyakazi)
Maadhimisho yataanza saa tatu asubuhi mpaka saa saba mchana
Imetolewa na Mganga mkuu wa kituo cha afya chuo kikuu cha
mkwawa (Dr Simon Lyuba).
MNAKARIBISHWA SANA WANAJUMUIYA YA CHUO KIKUU CHA MKWAWA
No comments:
Post a Comment